IMPORTANT! Kuna njia ngapi za kukuza biashara? 3!

Discussion in 'Masoko na Promosheni' started by Brainiac, Jan 4, 2018.

Share This Page

Watchers:
This thread is being watched by 1 user.
 1. Brainiac
  Offline

  Brainiac Staff Member Administrator Super Moderators Support Members

  Reputations:
  120
  Joined:
  Sep 27, 2017
  Messages:
  73
  Likes Received:
  148
  Liked:
  31
  Trophy Points:
  37
  Gender:
  Male
  Location:
  Arusha
  Credit:
  $1,730,756.20
  Kwa kuwa ni mwanzo wa mwaka mpya, nadhani ningependa kushare kidogo haya muhimu ambayo wengi wetu kama wahitaji mafanikio tunayajadili sana,

  You see, ni rahisi sana siku hizi kusimamia na kendesha biashara yako - mtandaoni na nje ya mtandao kuna maelfu ya fursa ya "kusimamisha jina la biashara yako kwenye masoko"

  Lakini kuna njia tatu muhimu za kufanyia kazi katika mafanikio ya biashara yako kwenye soko (ila pia nitakubali mtu yeyote ambaye anaweza kuja na ya nne!)

  • Wateja Zaidi:

  Rahisi, huh? Pata wateja zaidi na utatengeneza fedha zaidi. Lakini kufanikiwa katika "biashara mpya" mara nyingi ina gharama kubwa na inahitaji muda kuliko kuweka fedha katika benki.

  • Ongeza thamani ya mauzo:

  Je! Unaweza kufanya nini ili watu waweze kutumia pesa nyingi wakati wanapofika kwenye mpaka" yako? (biashara yako), Ubora wa bidhaa, na kuuza bei nzuri pasi na kuangalia faida kubwa! Umefanya kazi ngumu (ndio) kushinda mteja wako, ila hakikisha unawatumia vyema wateja waweze kutumia kiasi ambacho wanaweza na wewe utaridhia(watarudi kesho pia).

  • Ongeza thamani ya mauzo zaidi na zaidi:

  Ni mara ngapi wateja wako kwa wastani wananunua kutoka kwako kwa mwaka? Je, nini unafanya kuongeza idadi hiyo? Uaminifu wako kwa wateja, mawasiliano ya mara kwa mara kuhusu bidhaa mpya na mikataba ya ofa mbalimbali (silaha ya kufanikiwa kwa hili)

  Ila hapa ndipo maajabu hutokea, Je vipi kama utaweza kufanyia kazi njia hizo 3 japo kwa 10% tu? kwa wateja zaidi ya 10%, wakatumia fedha zaidi ya 10%, mara nyingi zaidi ya 10%? biashara yako itakua kwa asilimia 33.1! huhu!!!!! (sio Uchawi)

  Maudhui ya mada! Wakati mchezaji aanenelea kufurahia chezo (coz kwa kawaida hua ivyo pale mambo ya ubunifu yanapofanyika), hakikisha uuzaji wowote unaofanya una lengo la kufikia mojawapo ya malengo hayo matatu. Wateja zaidi, wanatumia fedha zaidi, mara nyingi zaidi.

  Hivi ndiyo biashara inakua- na ndio jinsi unaweza kutengeneza fedha zaidi mwaka 2018 kuliko ulivyofanya mwaka 2017.

  Have fun doing it!
  #MjasiriamaliDesk
   
  Eliezer and success like this.

Share This Page