Featured Ushauri BIASHARA YAKO INAHITAJI KUWA NA WASIFU WA UWEZO (CAPABILITY STATEMENT)

Discussion in 'Biashara na Ujasiriamali' started by imani soko, Jan 8, 2018.

Share This Page

Watchers:
This thread is being watched by 1 user.
 1. imani soko
  Offline

  imani soko Support Members Founding Member

  Reputations:
  29
  Joined:
  Nov 28, 2017
  Messages:
  27
  Likes Received:
  54
  Liked:
  0
  Trophy Points:
  17
  Gender:
  Male
  Location:
  dodoma
  Credit:
  $35,868.25
  Kila mtu mwenye kuhitaji ajira Anajua umuhimu wa kuwa na WASIFU binafsi (cv). Pamoja na barua ya maombi kila muajiri anahitaji pia kila muombaji awasilishe pia WASIFU wake. WASIFU humpa nafasi muajiri kumfahamu vizuri muombaji kabla hata ya kukutana uso kwa uso.

  Kupitia WASIFU wako muajiri atapata taarifa muhimu zinazohusu umri wako, asili yako, elimu yako, hadhi yako kifamilia, ujuzi ulionao, uzoefu wako wa kazi, nakadhalika. Kwa sababu hii watu wajanja huwekeza raslimali ya muda na fedha kuhakikisha kuwa wanakuwa na WASIFU unaoweza kuwauza vizuri kwa waajiri.

  Kama ilivyo kwa watu binafsi, Biashara binafsi na kampuni nazo huwa zinaomba kazi. Kuna wakati zinaomba kazi kama matokeo ya kutambua fursa fulani ndani ya serikali, taasisi nyingine, au hata watu binafsi.

  Aidha inapotangazwa zabuni, biashara binafsi/kampuni huingia katika ushindani kila moja ikilenga kushinda zabuni husika. Kwa bahati mbaya mara nyingi biashara binafsi/kampuni hazioni umuhimu wa kuwa na WASIFU mzuri unaoweza kuwasaidia kujiuza kwa watoa kazi. Kutokana na hali hiyo biashara binafsi nyingi na baadhi ya kampuni zimejikuta zikishindwa kupata kazi za kutosha na hivyo kuwa katika mdororo usiokwisha.

  Kuwekeza kwenye kuwa na WASIFU mzuri wa biashara/kampuni ni kitendo muhimu kwa uhai na ustawi wa biashara yako au kampuni yenu.

  Iwapo utahitaji msaada katika suala hilo unaweza kuwasiliana nasi. Kwa gharama nafuu kabisa tutakuandalia WASIFU wa biashara/kampuni yako ambao utaiweka biashara/kampuni yako katika nafasi ya kutazamwa vizuri na wadau wako mbalimbali wa kibiashara.
   
  Eliezer and Humflin like this.

Share This Page